Ronaldo Luís Nazário de Lima aliyezaliwa miaka 41 iliyopita katika jiji la Rio de Jeneiro nchini Brazil amefanikiwa asilimia 51 ya umiliki katika timu inayoshiriki katika ligi kuu nchini Uhispania Laliga ambayo ni Real Valladolid.
Mkongwe huyo ambaye alishawahi kuichezea ligi hiyo kubwa duniani kwa zaidi ya miaka 6 akizitumikia klabu za FC Barcelona na Real Madrid huku akistaafu soka mwaka 2011,akichezea timu yake ya taifa kwa zaidi ya miaka 16 akiifungia magoli 62 na kuichezea michezo 98 ameamua kujiingiza kwenye biashara hiyo kubwa kwa sasa duniani kwa kuamua kuinunua klabu ya Real Valladolid.

